Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Karatu jioni ya leo,
ambapo aliwasihi wananchi wa wilaya hiyo ambayo inaoongozwa na Chadema,
kuachana nacho kwani kwa muda wa miaka kumi na mitano iliyoongoza hakuna
maendeleo yoyote waliyowaletea zaidi kutumia ovyo fedha zinazopekwa na
Serikali wilayani humo kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Halmashauri ya
Wilaya hiyo inaoongwa na Chadema.
Kinana ambaye yupo mkoani Arusha kwa
ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi
na kuzitafutia ufumbuzi, alishuhudia Halmashauri ya Karatu inayoongozwa
na Chadema imekataa kutoa sh. mil 60 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa
ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Baray Mbuga Nyekundu, kisa Kata
hiyo inaongozwa na Diwani wa CCM. |
No comments:
Post a Comment