Muonekano wa kontena lililosababisha ajali hiyo.
"Wazazi wa mtoto waliingia na kukaa
siti ya tatu tu kutoka kwa dereva. Hakuna aliyehisi kwamba mbele ya
safari kuna janga kubwa kama hili."Basi lilianza safari, kila abiria
alikuwa akizungumza na mwenzake, wengine walikuwa wakiongea na simu.
Wapo waliokuwa wakichati, nadhani ni wale wanaotumia WhatsApp. Kumbe
bwana shetani alikuwa anatembea na sisi," alisema abiria huyo akiwa
kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mufindi.
KABLA YA AJALI Kwa
mujibu wa majeruhi mwingine wa ajali hiyo, baada ya kufika eneo la
Changarawe, kwa mbele lilionekana lori hilo likiwa katika mwendo wa
kawaida na hakuna aliyewaza kwamba litaangukia basi lao.
"Mbele tuliliona lile lori likija,
lakini mimi nimekuwa nikisafiri mara kwa mara kwa kutumia barabara hiyo.
Najua eneo hilo lina shimo lakini sikuwa na wazo kwamba shimo lile
litakuwa mtoa roho wa abiria wa basi letu. "Wakati
tunapishana sasa, lori linapita kulia kwetu, mimi nilikaa siti ya nyuma
upande wa abiria. Ghafla nilishtuka kuona kama giza linatanda upande wa
dereva, mara nikasikia watu wakianza kulia.
"Kabla sijajua ni nini, nikasikia
kishindo kikuu. Puuu! Abiria wengine walisikika wakisema wanakufa,
wengine wakiwa kimya! Ndipo nikajua tumeangukiwa na kontena lakini
sikuweza kufuatilia ilikuaje kwani akili zikawa kama zimeniruka,"
alisema abiria huyo bila kutaja jina lake. |
No comments:
Post a Comment